MARAFIKI ni watu Muhimu sana katika maisha ya
kawaida. Kuna muda huwa tunakutana na watu mbali mbali ambao huwa tunawafanya
kuwa marafiki kulingana na Muonekano, tabia, Historia za Kimaisha, na
mengineyo.
Kuna ukweli kwamba, kuna marafiki ambao huwa
wanakubali kile ambacho unakifanya, na hata kujivunia kuwa karibu na Wewe, ili
kufanikisha Suala hilo, ama Kukupa Ushauri mzuri na hatimaye kufikia pazuri.
Lakini Pia kuna marafiki ambao huwa
hawatabiriki. Leo anakupenda, kesho anakuchukia, Wiki ijayo anapenda
ushirikiano wako, Wiki nyngine hataki umuingilie katika mambo yake, lakini kuna
muda hataki hata kukusikia.
Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba huyo bado
ni rafiki ako, na unatakiwa ufanye yafuatayo:
- · Muamini katika kila anachokifanya
- · Mpongeze katika mafanikio anayofikia.
- · Mkumbushe mambo ya Msingi ambayo huenda ameyasahau.
- · Kuwa Mstari wa Mbele katika kufanikisha Kazi yake, Yaaluma, Kipaji, na hata Shughuli zake
- · Kumbuka Kujishusha Chini unapobaini hayuko katika Mood Nzuri
- · Mshirikishe katika Baadhi ya mambo yako ya Msingi hata kama hatofurahishwa nayo
- · Kubali ushauri wake, na kuuboresha Kama Una mapungufu.
- · Mheshimu, na uthamini utu wake, huku ukiepuka Kuhisi Mambo mabaya Juu yake.
- · Kuwa wa Kwanza Kumuombea kwa Mungu ili awe na maisha Bora
- · Mfanyie Kitu Kizuri ambacho hakiamini kama unaweza kukifanya.
- · Kubali na Pokea Lawama, Matusi, hasira, Chuki na Mengine, kutoka kwake dhidi yako.
- · Onyesha Furaha kila siku unapokutana naye, na epuka kumlaumu pindi asipozingatia Salamu yako, Ushauri wako, na hata anapokuona huna mchango wowote katika Maisha yake
EmoticonEmoticon