KOCHA wa Timu ya Taifa ya MEXICO, amewapiga
marufuku wachezaji wa Timu yake Kushiriki Tebndo la Ndoa katika kipindi cha
mashindano ya Kombe la dunia Mwaka huu Nchini Brazil.
Akizungumza na Gazeti la REFORMA, Kocha Huyo
amedaiwa Kuwaagiza wachezaji wake kutokujihusisha na Suala la kufanya mapenzi,
na badala yake wanatakiwa kujikita zaidi na kuelekeza Macho yao katika Soka
hasa Michuano Hiyo ya Dunia
Aidha Kocha huyo anayetambulika kwa Jina la
MIGUEL HERRERA, ameongeza kuwa, kama Mchezaji hatovumilia kutokufanya mapenzi
kwa Mwezi Mzima ama Siku 20, basi hajajiandaa kuwa Mchezaji Professional.
Mexico Inatarajia Kukutana na Timu ya Brazili
katika Kundi A, pamoja na Coratia na Cameroon
EmoticonEmoticon