HIVI MAJUZI TU, TULIPATA TAARIFA
NZURI KUWA, CHRIS BROWN AMBAYE HIVI SASA
BADO ANAKABILIWA NA KESI YA KUMCHAPA MAKOFI RIHANNA MIAKA KADHAA ILIYOPITA,
AMEANZISHA TAASISI YA MASUALA YA UREMBO NA MITINDO, JAMBO AMBALO WENGI
WALIMTAKIA KILA LA KHERI POP SINGER HUYU…
Lakini janga linguine limeikumba
taasisi hiyo baada ya Mrembo mmoja kudai kuwa Wanaitumia picha yake katika
matangazo ya kibiashara pasipo kumlipa.
STASIYA MARIA anadai kuwa, yeye
alipewa Mualiko wa kuhudhuria katika zoezi la jaribio la Upigaji Picha Mnamo
March 21 Mwaka huu, huku baadaye akiingizwa katika hatua nyngine ya zoezi hilo,
pasipo kufahamu kinachoendelea, huku akipiga mapoz Mwanana na warembo wengine.
Aidha Maria ameendelea kumiminika
kuwa, hajawahi kupewa Mkataba wowote na Taasisi hiyo, na jambo la kushangaza ni
kwamba, hivi sasa anatumika katika Promotion za Angency ya Chris Brown kupitia
Mitandao ya Instagram, hata Bila malipo.
Aidha Mpaka hivi sasa, TTM tumethibitishiwa kuwa, Mwanasheria Wa Maria ameiamuru taasisi hiyo ya Chris Brown Kuondoa video na Picha ambazo zinasambazwa katika Mitandao yote ya kijamii, bila Hivyo, watafungua mashtaka
EmoticonEmoticon