LUDA CRISS safari Hii amekumbana na Misukosuko
Mikali ambayo huenda ikamfanya akapata athari hasa Kisaikolojia, endapo
hatokuwa makini.
Miezi kadhaa iliyopita, rapper Huyo kutoka
ATLANTA alifunguliwa mashtaka na Mzazi mwenzake, TAMIKA FULLER, kwa madai ya
kushindwa kumhudumia mtoto wao ambaye walikubaliana kumpatia Kiasi kadhaa cha
fedha kwa ajili ya matumizi mbali mbali.
Lakini katika Utetezi wake, Ludda alidai kuwa
hakuwa Vizuri kifedha, baada ya Kifo cha Paul walker kusitisha Zoezi la
Utengenezwaji wa Filamu ya FAST AND FURIOUS 7 , aliyokuwa akiitegemea kwa hali
na Mali.
Sasa, hivi majuzi TTM tumezinyaka Kuwa, Hitmaker
huyo wa WHAT THEM GAL WANTS alifungua mashtaka Dhidi ya Mzazi Mwenzake huyo,
kwa kuvujisha Nyaraka za Mahakama ambazo Kimsingi hazikutakiwa kufikishwa
katika mitandao mbali mbali ya kijamii kama ambavyo iliamriwa na Mahakama.
Kwa mujibu wa madai ya LUDA akiwa mahakamani,
alisema kuwa, TAMIKA alivujisha Nyaraka Hizo katika Mtandao wa Kidaku zaidi
nchini marekani, MEDIA TAKE OUT.COM, na Ushahidi alikuwa nao kabisa.
Baada ya Hakimu kupitia Ushaihidi huo, bado
alipiga Chini madai ya Luda katika mahakama hiyo ya FULTON COUNTY, huku
akimuamuru Luda Kumlipa Mwanasheria Wa TAMIKA kwa usumbufu aliousababisha.
EmoticonEmoticon