“Ukinikosea Heshima Nitaitafuta Kwa Nguvu” hiki
Ndicho alichokithibitisha Star wa Nigeria, D’BANJ-“THE COCO MASTER” himself.
Akizungumza kunako Moja kati ya Interview Nchini
Nigeria, D’banj maesema kuwa ameamua kufikia hatua baada ya DAILY MAIL
kumchafua na hata Kumharibia Sifa yake, kwa Kuandika kuwa Yeye Ni Mtu wa Totoz,
yaani anapiga na kuacha.
Katika ufafanuzi wake, D’banj ameongeza kuwa
hivi sasa anajadiliana na Wanasheria wake ili kuweka kila kitu sawa, na
hatimaye kuweza kufuata taratibu za Kisheria na kukamilisha Mchakato mzima wa
kufungua Mashitaka hayo.
Aidha Mkali huyo wa OLIVER TWIST ameongeza kuwa
habari Ile haikuwa na ukweli wowote kuhusu maisha yake na hata tabia yake,
kwani yeye hana Mwenendo huo, kwa kuwa anawaheshimu wanawake.
Tofauti na Hilo, D’Banj aliongeza kuwa, katika
uandishi huo hasa katika hiyo Stori yake, DAILY MAIL hawakufanya hata mahojiano
naye kuhusu Tabia waliyompakazia. Hivyo walimzungumzia Kokomaster Vibaya,
ingawa anahisi walitaka kumzungumzia KENYA MOORE kwa kile kilichodaiwa
kubiringika naye, lakini hawakumtafuta D’banj Mwenyewe ili Kuweka Usawa.
Kuhusiana na Suala la mapenzi Kwake hasa
mahusiano aliyonayo hivi sasa, D’banj amedai kuwa hivi sasa ana Mpenzi
anayempenda kwa Dhati, na atamuoa Siku ambayo atakuwa tayari.
EmoticonEmoticon