KAMA UTAKUWA NI MDAU
MZURI TU WA RAPA 50 CENTS, TTM INAAMINI UTAKUWA UNAFAHAMU KUWA RAPA HUYO YUKO
NDANI YA “BIG” BEEF NA KAMPUNI YA SLEEK AUDIO KWA MADAI YA KUIBA DESIGN YA
HEADPHONES PAMOJA NA BAADHI YA DATA AMBAZO ZILIKUWA ZINATUMIKA KISIRI SIRI
TTM tumenyaka Updates
kuwa Ishu hiyo ama Kesi hiyo ilikuwa ikiendelea, na Kwa mara nyingine tena,
RAPA FIF amejikuta akishindwa katika Kesi hiyo ambayo Wengi wanaamini
ilimuumiza Sana kichwa.
Mnamo 2013, 50 Cents
aliifungulia mashtaka Kampuni hiyo ya SLEEK AUDIO huku akilalamika Kuwa,
anaidai kampuni hiyo jumla ya DOLAR za kimarekani 261,000, lakini Mwisho waSiku
majibu yalikuja tofauti baada ya FIDDY kushindwa kwa mara ya Kwanza kabisa.
Kwa mujibu wa Kitengo
cha Chimbua Chimbua, 50 ameamuliwa na mahakama Kuilipa kampuni hiyo kiasi cha
USD Milioni 16.1 kwa Kosa la kutumia Designing ya kampuni hiyo pamoja Baadhi ya
Data kutoka katika kampuni Hiyo hiyo, bila taarifa Maalum.
SLEEK AUDIO waliongeza
Kuwa, awali walitakiwa kushirikiana na RAPA huyo wa Track ya PILOT, lakini
baada ya Kushindwana katika makubaliano yao, walishangaa kuona Designing zao na
Vitu vingine vikitumika katika Headphone hizo za 50 CENTS.
Licha ya Kutumia
vibaya baadhi ya vitu vyao pasipo makubaliano hasa ya Kifedha, kampuni ya SLEEK
AUDIO pia Imesema kuwa 50 na Msaidizi wake, waliiba na Kutumia Baadhi ya
maelezo kutoka katika WEBSITE yao Bila idhini yoyote, jambo ambalo ni Kinyume
na taratibu za Kibiashara, na ni uharibifu wa Soko lao.
Mpaka hivi sasa,
mahakama imemuamuru 50 Cents ambaye jina lake halisi ni JACKSON CURTIS, kiasi cha USD 11,693,247 kwa ajili ya
Uharibifu, pamoja na USD 4,488,331 kama malipo ya Usumbufu kwa Mwanasheria wa
SLEEK AUDIO
EmoticonEmoticon