KIUKWELI Hata Mie Nilishtuka kuona info hii
kutoka Nchini Kenya, but Honestly ninajivunia Kile ambacho WAHUU amekizungumza
katika Moja ya Interview Nchini Humo.
Wahuu ambaye alishika sana akili za Mutu Nyingi
kupitia kwaju la SWEETLOVE, alifunguka na kujibu swali ambalo aliulizwa kuhusu
Mzazi halali wa Mtoto wao Mpya wa kike, NYAKIO.
Katika maelezo yake, WAHUU amesema kuwa,
NAMELESS Ndiye baba wa Mtoto na atabaki kuwa baba wa Mtoto wao huyo.
Pia Wahuu aliongeza kuwa, ni kweli kuna muda
ilitokea mikwaruzano katika Ndoa, kama ambavyo hali inavyoweza kutokea kwa
wanandoa wengine, lakini yale ni matatizo madogo tu ya kutokuelewana, na hata
siku moja hawakuwahi kufikiria suala zima la Taraka au Kuachana.
Pia Wahuu aliongeza kuwa, kuna baadhi ya Vitu
ambavyo wao kama wanandoa walikuwa wakijikuta hawakubaliani navyo na
kutofautiana, lakini hawakuwahi kumaliza Wiki au Mwezi pasipo kuongeleshana ama
kusalimiana, kama ilivyo kwa Wengine ambao hudiriki hata kumaliza Mwezi
hawasalimiani, licha ya kwamba wanaishi Pamoja
EmoticonEmoticon