ULALALAAAAA….
Chochote Kinachotuhusu Lazima
TTM tukupe Mtonyo kama kawaida, sasa Iko Hivi
RAPA Kutoka kunako Jiji la
CHICAGO, Nchini marekani, Kanye West, usiku wa kuamkia leo aliingia kunako
danger Zone yake baada ya kujikuta akiwa amezungukwa na watu anaowachukia
kupita kitu chochote, yaani mapaparazi.
Unaweza kujiuliza ni hatua gani
ambayo YEEZY aliichukua maana huwa anapiga Ngumi na mateke pale anaposumbuliwa
na Mapaparazi hao, lakini hali hiyo ilikuwa tofauti kutokana na kutumikia
kifungo Cha Nje cha Miaka miwili, baada ya kukutwa na hatia ya kumpa kipigo
Mpiga Picha Mmoja huko LOS ANGELS.
Tukio hilo lilitokea katika
uwanja wa Ndege huko huko Nchini Marekani, ambapo baada ya kutoka tu maeneo ya
Nje, alikutana na nyomi hilo la wana habari, huku mmoja wa Wapiga picha hao
kutokea TMZ akimuuliza swali kuhusu Picha yake na Kim Kardashian Kuonekana
kwenye Front Cover ya jarida la VOGUE.
Licha ya Kuulizwa maswali mengi
sana na wapiga picha hao huku Upigaji Picha ukiendelea, Kanye West bado
alionekana kuwa Mdogo kama Pilitoni, na kugoma kujibu Kila swali ambalo liliulizwa
maeneo hayo.
EmoticonEmoticon