Kama utakuwa ni Mtaalamu mzuri wa kucheza na
Info za Mastaa mbali mbali, Kuna Muda Fulani hivi zilivuma kuwa Huenda Diamond
akawa anamfukuzia msanii hatari wa kike nchini Kenya, VICTORIA KIMANI, jambo
ambalo Platnumz alilipinga kabisa na
kudai ni marafiki.
Sasa katika pita yetu huku na kule, tukabaini
kuwa Bamboo Pia ambaye ni kaka wa Victoria Kimani, amevunja ukimya pia na
kulitolea ufafanuzi Suala hilo ambalo limezagaa sehemu kibao hasa katika
Mitandao ya Kidaku.
Katika ufafanuzi wake, BAMBOO amesema kuwa Mdogo
wake huyo mrembo, sio Type ya PLATNUMZ, lakini kama atafikia uamuzi wa kuingia
katika mahusiano na Diamond, basi yeye hawezi kumzuia coz ni binti ambaye Yuko
huru, na anaweza kufanya maamuzi yake.
Aidha bamboo aliongeza kuwa, Victoria amekuwa ni
binti mtafutaji kuanzia muda mrefu, lakini pia amekuwa akishiriki katika nyimbo
kadhaa za Nchini Kenya ingawa watu wengi hawafahamu.
Ishu ya Diamond kuhisiwa anachoporoka na
Victoria Kimani, ni baada ya kupost picha yake na mrembo huyo katika Pozi la
kawaida Tu, wakati wako katika Project ya Kutengeneza kwaju la ONE CAMPAIGN
EmoticonEmoticon