HATA KAMA NI DRAMA , lakini kubali ukatae, The
Show Must Go on ili tujue kipi ambacho kinablink kunako Burudani na wahusika wa
burudani
Iko Hivi,Wengi tunafahamu kuwa MUSTAPHA na MARYA
walikuwa ni wapenzi ambao walionekana kushibana, lakini Suala la Dini Ndilo
lililokuja kuwafanya wasifikie malengo ya Mipango yao hasa katika Suala Zima la
kuishi pamoja.
Kama utakuwa umepoteza Memory kidogo, Marya
alitakiwa abadilishe Dini kutoka kunako UKRISTO mpaka Kuwa Muislam ili aweze
kumatch na MUSTAPHA ambaye ni Muislam, lakini jambo hilo lilishindikana, na
hatimaye marya akasepetuka kutoka katka Nyumba ya Mustafa, huku Sababu ya
Danganya toto, ikiwa ni kupeana Likizo.
Sasa baada ya Kumwagana huku Mustapha akifanya
Jitihada ili kumrudisha Marya katika maisha yake, mambo yakaenda Ndivyo sivyo
na hatimaye kuangukia kunako mikono ya Aliyekuwa mwakilishi wan chi ya Kenya
katika Shindano la BIG BROTHER AFRICA 2013, Huddah, na mambo ndo yakaanzia
hapo…
Baada ya kupata hizo Drama za kutosha, TTM
tuliamua Kuzama ndani na kutafuta marya anazungumziaje uhusiano wa HUDDAH na
MUSTAPHA, lakini Full info ni kwamba, Marya amesema anajiskia kawaida sana
kuhusu uhusiano huo, na wala hakuwa anafahamu chochote kuhusu wawili hao, maana
alikuwa Busy na Mishe zake za kibiashara na maisha kiujumla.
Hata Hivyo Amefunga kila kitu kwa kusema kuwa,
amefurahi kusiki wawili hao wanapendana kwa dhati, na anawatakia maisha yenye
furaha katika safari yao ya mapenzi
EmoticonEmoticon