TTM Leo tumebaini kuwa Kumbe Chris Brown na
aliyekuwa Mpenzi wake Rihanna, bado wako In Touch na Kuna Kila aina ya Dalili ya
kurudisha mahusiano yao ya kimapenzi.
Kama utakuwa ni Good member wa TTM, jana
tulikupa Mtonyo kuwa Drake anaweza kuwa ni Mwanaume ambaye anamfanya Rihanna
afurahi, kumbe WaaaalaaaH, Rihanna anamchora tu Kijana wa Watu.
Chanzo Kilichopo karibu na Rihanna, kimedai kuwa
Tangia Breezy atoke Rehab alikopiga Siku 90, ili kumsaidia kucontrol hasira
zake, amekuwa akichat mara kwa mara na Chris brown , jambo ambalo Rihanna
ameonekana kulifurahia kwa Kiasi Fulani.
Aidha chanzo hicho kimeongeza kuwa Breezy
ameanza kumtext, yaani kumtumia Messeji Rihanna, tangu alipokuwa akisherehekea
Birthday yake ya kutimiza miaka 26.
Tofauti na hilo, inasemekana kuwa RIRI ambaye ni
Mkali wa DIAMONDS, awali hakujibu meseji za Chris Brown, lakini kadri Muda
Ulivyokwenda, RIRI alipata hamasa ya Kumjibu na hatimaye kumwandikia maneno
kama AHSANTE, na Kisha akamuuliza Chris Brown alikuwa akiendeleaje huko Rehab.
Katika Kuongeza hilo, Chris Brown na Mpenzi wake
wa sasa Karrueche, hawako pamoja kama marafiki wanapatikana katika account ya
Twitter, tofauti na ilivyokuwa Awali.
EmoticonEmoticon