KAMA Kuna watu ni wasiri kabisa katika Suala la
Mipango ya Ndoa, basi KANYE WEST na KIM KARDASHIAN wanaongoza.
Lakini Kwa Upekuzi wetu wa KIBISHI, TTM tumepata
Mtonyo Kuwa Wawili hao Wanampango wa Kufunga Ndoa yao rasmi Mbnamo JUNE Mwaka
Huu.
Kwa Mujibu wa Chanzo ambacho kipo karibu sana na
Wawili hao, Inasemekana Kuwa, KIM KARDASHIAN amekuwa akimshawishi sana KANYE
wfunge Ndoa yao katika Mwezi Huo, Ombi ambalo lilifanikiwa Kwani Inaonekana
KANYE Huwa hakatai Chochote kwa Mzazi Mwenzake Huyo.
Licha ya Kuinyaka Hasa kuhusu Mwezi wa Ndoa,
bado Mpaka hivi sasa, wawili hao hawajamvujishia Mtu Yeyote Mahali ambako
watafungia Ndoa yao, ingawa Awali wawilio hao walisadikika kutaka kufunga Ndoa
Yao katika Eneo Linaloitwa VERSAILLES Huko Nchini Ufarasa, baada ya wawili hao
kutembelea Eneo Hilo.
EmoticonEmoticon