KUSEMA Kweli, Si Stori Nzuri ya Kufurahisha wala
Kuburudisha, Bali Inaumiza na Kusikitisha Kwa Mtu yeyote Mwenye Akili Timamu,na
anayejielewa kama TTM Ilivyo.
MAMA wa Watoto wawili, amekutwa hatiani kwa
Kusababisha Kifo Cha watoto Wake wawili Baada ya kuwafungia Ndani ya gari na
Kuwaacha katika Joto kali, na Kwenda kwenye gari jingine kwa ajili ya Kufanya
mapenzi.
Binti Huyo HEATHER JENSEN Mwenye Umri wa Miaka
25, alifanya Tukio Hilo Mnamo November 27, 2012, na Kusababisha Kifo cha watoto
hao ambao Walipoteza maisha Ndani ya gari kwa Kukabiliwa na Joto Kali.
Hakimu wa Kesi Hiyo DANIELLE LEWIS, alisema
kuwa, Hukumu ya kifo Inamkabili Kwa nafasi Kubwa Miss Jensen kwa Kosa Hilo,
kwani inajidhihirisha kabisa kuwa aliandaa mazingira ya Kifo cha watoto hao, huku
akikabiliwa Na Shitaka Lingine la Ukatili Wa Watoto.
Aidha WAKILI anayemtetea Miss Jensen, amedai
Kuwa, Tukio Lililotokea Siku Hiyo, halikuwa Makusudi na Wala halikupangwa, bali
lilitokea kama Ajali, hivyo hatakiwi Kuhukmiwa hukumu kali ambayo hata yeye
hakustahili Kuipata.
Akitoa Ufafanuzi kuhusu hali iliyojitokeza,
Mtuhumiwa anasema kuwa NOVEMBER 27,2012, alitoka na watoto wake hao wawili,
WILLIAM Mwenye Miaka 2 na TYLER Mwenye Miaka 4 kuelekea Sehemu ambako Kuna
barafu kwa ajili ya Kucheza na Kufurahia, na kama Bahati, alikutana na huyo
Boyfriend wake Mpya, ambaye walikubaliana Kufanya Tendo La Ndoa Huko Huko.
Miss Jensen aliongeza kuwa, Kwa mara ya Kwanza,
wakati wako katika Raha zao, baada Ya dakika 30, TYLER ambaye Ni Mkubwa,
alifungua Mlango wa Gari la mama yao na kutoka Nje, lakini Mtuhumiwa
alimrudisha Tena, huku akimpatia Simu ili achezee, Kisha akafunga Mlango kwa
LOCK, akawawashia AC na Kuweka Joto, kisha akarudi kwa huyo Jamaa ake.
Inasemekana kuwa watoto hao walikaa Ndani ya
gari Hilo kwa Muda wa Dakika 90, huku ikiaminika Kuwa, huenda Joto liliongezeka
sana Mpaka Kufikia DEGREE 60, na Kusababisha Kifo Chao.
Akizidi kuhimiza Utetezi Kwa mtenja wake, wakili
wa Mtuhumiwa amesema Kuwa, Uchunguzi zaidi ungefanyika, anakabiliwa na Matatizo
mbali mbali hasa Kiakili, yaani IQ yake ni Ndogo, Umri wake kuwa Mdogo, na
huenda alikuwa katika Kuchanganyikiwa baada ya
Kumpoteza Mume wake, Wiki Sita kabla
ya tukio.
Kwa upande wake Jamaa ambaye alikuwa akifanya
mapenzi na Mtuhumiwa, alidai Kuwa, Ms Jensen alikuwa amevuta Bangi Siku Moja
kabla Ya Tukio la Kifo cha watoto Wake.
Kesi Hiyo itasikilizwa kwa Muda wa Siku Tisa na
Hatimaye Hukumu Kutolewa.
EmoticonEmoticon