Vikosi vya jeshi la Mali hii leo vimeelekea kwenye mji wa
kaskazini mashariki wa Kidal ikiwa ni kabla ya muda uliopangwa na serikali wa
kuukomboa kutoka katika mikono ya waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga
Vikosi vya Ufaransa vilivyokuwa vikipambana na waasi
kaskazini mwa Mali viliwaruhusu waasi wa MNLA kudhibiti mji wa Kidal katika
miezi ya hivi karibuni, lakini serikali ya Mali inataka kuudhibiti mji huo
kabla ya uchaguzi wa rais na Bunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai. Waziri
wa Ulinzi wa Yamoussa Camara alisema bungeni mwezi huu kwamba, swali kuhusiana
na kudhibitiwa mji wa Kidal na waasi wa MNLA litajibiwa ifikapo Mei 15.
Waasi wa MNLA walikataa wito wa serikali ya Bamako wa kuweka
chini silaha, wakisema kuwa watakabiliana na jitihada zozote za serikali za
kudhibiti tena mji wa Kidal, lakini walisema mlango wa mazungumzo ya kisiasa na
serikali upo wazi.
Katika upande mwingine Rais wa Chad ametangaza kuwa, askari
wa nchi hiyo waliokuwa wakipigana nchini Mali na makundi ya waasi, wanaanza
kurejea nchini kwao.
EmoticonEmoticon