WANAFUNZI zaidi ya ishirini wenye umri wa kati ya miaka 7 -
9 wa shule ya kimataifa ya St Charles
iliyopo Don Bosco katika Manispaa ya Iringa wamenusurika kifo baada ya gari
waliyokuwa wamepanga lenye namba T415AEG kushindwa kupanda mlima na kupinduka.
Ajali hiyo imetokea jana mchana katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata
ya Mvinjeni katikati ya mji wa Iringa.
Walioshuhudia tukio hilo
wamesema daladala hilo lilikuwa likitokea eneo
la FRELIMO katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa na baada ya kufika
eneo hilo
lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma kwa kasi kabla ya kupinduka.
Alisema shuhuda, Juma Omari kuwa chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa dereva ambaye alionekana kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari pamoja na
kutambua kuwa mbele kuna kona na mlima.
Anasema, wananchi walitoa msaada wa kuwatoa katika daladala
na kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya
mwanamke mmoja ambae jina lake
bado kufahamika
aliyejeruhiwa vibaya mikono yake.
Mmoja kati ya wauguzi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa ambae
hakutaka kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Hospitali hiyo alisema kuwa hali
za watoto hao si mbaya sana
zaidi ya kupata michubuko midogo midogo.
EmoticonEmoticon