Baada ya taarifa kuenea kuhusu uwepo wa msanii Dogo Janja
nchini Afrika Kusini kwa show alizopata zilizofanyika ndani ya wiki tatu,
Uongozi wa shule anayosoma ya Makongo Sekondari, umetoa taarifa kuhusu mwenendo
wake pamoja na matokeo aliyopata ya kidato cha pili.
Michael Alfred Mbaula ambae ni Afisa taaluma amesema
“mahudhurio ya Dogo Janja darasani yalikua mazuri na alikua anashirikiana
vizuri na wenzake kipindi kilichopita ila mara yake ya mwisho kuingia darasani
ni novemba 2012, na kwa sasa atalazimika kurudia kidato cha pili kwa sababu
amefeli kwa wastani mdogo ambao usingemruhusu kuendelea na kidato cha tatu”
Kuhusu kauli ya Dogo Janja kwamba juzi alipokwenda Afrika
Kusini alikua ameomba ruhusa ya wiki mbili shuleni, Mbaula amesema “sio kweli
kwamba aliomba ruhusa na wala ofisi haina taarifa japo shule haina tatizo
akitoa taarifa hata katikati ya masomo iwapo anatakiwa kufanya shughuli za
mziki kwa sababu Makongo ni shule ya vipaji, kuomba ruhusa ya wiki moja au
mbili ambazo alikua akiziomba mwaka uliopita ndani ya mwezi mmoja ni sahihi ila
kukaa miezi mitatu bila kuja shule ndio tatizo”
Mbaula amesema “Dogo Janja amefeli kidato cha pili kwa
kupata wastani wa 27 ambapo alifanya vibaya sana kwenye hesabu kwa kupata
sifuri, Civics alipata 27, historia 33, Jiografia 22, Kiswahili 46, Kiiingereza
42, Phisics 20, Chemistry 30, Biology 27, Commerce 8, Bookkeeping 11 hivyo ni
lazima arudie darasa kitu ambacho anaweza kukifanya hapahapa Makongo”
EmoticonEmoticon