UFARANSA na Uingereza zinajiandaa kuwapa silaha waasi wa
Syria hata bila kupata uungwaji mkono kutoka Umoja wa Ulaya.
Waziri wa mambo ya
nchi za kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius amesema Ufaransa na Uingereza zitatoa
wito wa kusongezwa tarehe ya mkutano ujao wa Umoja wa Ulaya utakaojadili
vikwazo vya usafirishaji silaha nchini Syria, na zitaamua kuwapa waasi zana za
kivita kama Umoja huo wenye nchi wanachama 27 hautaunga mkono suala hilo.
WAZIRI MKUU WA UFARANSA, LAURENT FABIUS
Fabius amekiambia kituo kimoja cha redio nchini Ufaransa kuwa nchi hizo mbili
zitauomba Umoja wa Ulaya kuondoa vikwazo vya silaha dhidi ya Syria ili waasi
wanaopambana kumwondoa madarakani Rais Bashar al-Assad waweze kujikinga.
WAZIRI MKUU WA UINGEREZA, DAVID CAMEROON
Mkutano ujao wa Umoja wa Ulaya utakaojadili vikwazo hivyo unapangwa mwezi
mwishoni mwa mwezi Mei, lakini Fabius amesema Ufaransa na Uingereza wanataka
mkutano huo uandaliwe mapema. Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron alisema
jana Jumatano kuwa Uingereza itazingatia kupuuza vikwazo hivyo vya Umoja wa
Ulaya na kuwapa silaha waasi wa Syria, ikiwa hilo litasaidia kumwondoa
madarakani Rais Assad.
EmoticonEmoticon