Baba Mtakatifu Francis wa kwanza, ambaye ndiye Papa wa
kwanza kuchaguliwa kutoka Amerika ya Kusini, leo amelitembelea kanisa moja
mjini Roma katika siku yake ya kwanza ya uongozi wake akilenga kulileta kanisa
katoliki karibu na watu.
Askofi huyo mkuu wa zamani wa Buenos Aires, Argentina,
mwenye umri wa miaka 76, Jorge (HORGE) Mario Bergoglio, amehudhuria misa ya
maombi katika kanisa la Santa Maria
(MAJIORE) Maggiore mjini Roma, ili kuanza kazi yake kama mkuu wa
wakatoliki bilioni 1.2 kote ulimwenguni. Wakati huo huo salamu za pongezi
zinaendelea kutumwa kutoka kote ulimwenguni.
Waziri Mkuu wa Australia Julia
Gillard amesema kuchaguliwa Papa kutoka "ulimwengu mpya" ni tukio
ambalo lina umuhimu wa kihistoria. Francis ambaye ndiye Papa wa kwanza
asiyetoka Ulaya katika kipindi cha takribani miaka 1,300, ameitumia ibada yake
ya kwanza kumwombea mtangulizi wake Benedict wa Kumi na Sita na kutoa wito wa
kuwepo udugu miongoni mwa waumini wa Kikatoliki. Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa Ban Ki Moon ametuma pongezi zake
EmoticonEmoticon