Mratibu wa Promosheni za Tigo Pesa
Mary Rutta akipiga simu kupata washindi watano wa shilingi milioni 10 katika
droo ya pili ya promo ‘Shinda Kitita na Tigo Pesa’ mapema leo. Wengine 20
walijishindia milioni 20 kila mmoja na wengine 350 walijishindia laki 2 kila
mmoja iliyofanya jumla ya shilingi milioni 160 kuzolewa. Katikati ni Meneja
Bidhaa wa Tigo Husni Seif na Msimamizi kutoka Bodi ya Michezo Tanzania Humudi
Abdulhussein.
JUMLA ya fedha taslimu shilingi
milioni 160 zimezolewa na wateja wa Tigo mara baada ya kampuni hiyo ya simu
kuchezesha droo yake ya pili katika promosheni yake ya ‘Shinda Kitita na Tigo
Pesa’ iliyofanyika mapema leo katika makao makuu yao Makumbusho jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari
wakati ya droo hiyo Mratibu wa promosheni za Tigo Pesa Bi. Mary Rutta alisema
kwamba wateja watano walijishindia milioni 10 kila mmoja, wateja wengine 20
wamejishindia shilingi milioni 20 kila mmoja na wengine 350 walijishindia
shilingi laki mbili mbili.
Washindi watano wa zawadi nono ya
shilingi milioni 10 ni Bi. Irene Francis
Mushi (25) mfanyabiashara wa vipodozi kutoka Moshi, Bi. Magadalena Daniel Asei
(37) mfanyakazi wa DHL mkazi wa Kigamboni – Dar es Salaam na Bi. Hilda Laurence
Nyambo (56) mfanyakazi wa kampuni ya Bima kutoka Kinondoni, Dar es Salaam.
Wengine ni Bi. Maria Juma Mbata (26)
mhitimu wa Chuo Kikuu mkazi wa Iringa na Bw. Aloyce Idrisa Njole (23)
mwanafunzi wa chuo cha ufundi anayetoka mkoani Morogoro.
“Tigo inafuraha kubwa sana kwa sababu
imeweza kuleta tabasamu katika nyuso za wateja wake katika kipindi hiki cha
mwaka mpya. Tunaamini kwamba zawadi hizi zitawafurahisha na kuwafanya
washerehekee sikukuu hii ya kuuaga mwaka 2013 kuingia 2014 kwa namna ya
kipekee,” alisema Bi. Rutta.
Aliongeza, “Kwa ujumla zawadi
zilizoshindaniwa leo ni milioni 50 kwa washindi watano waliopatikana, milioni
40 kwa washindi 20 na milioni 70 kwa washindi 350 ambapo kila siku wateja 50
walikuwa wanajishindia shilingi laki 2 kila mmoja, iliyofanya jumla kuwa shilingi
milioni 160.”
Kwa mujibu wa Mratibu huyo wa
Promosheni droo hii ilikuwa ya kuanzia tarehe 24 hadi 30 Desemba.
Utaratibu wa shindano hili unaruhusu
wateja waliosajiliwa na Tigo Pesa kushiriki katika promosheni hii kwa kutuma
fedha, kununua bidhaa kupitia Tigo Pesa, kutoa fedha, kununua muda wa maongezi
au kulipia huduma mbali mbali kupitia Tigo Pesa.
EmoticonEmoticon