Ikiwa Ni Siku Juma Moja Tu limepita
tangia KANYE WEST azungumze hadharani kuwa hatozungumza baya Lolote kwa Mtu
yeyote Mwaka 2014, Finallly Mabeste wawili wanaounda kundi la GOODLIFE, Radio
na Weasel nao wametoa tamko lao Rasmi….
Wakali hoa kutokea The Kaguta land
(UGANDA), wamesema kuwa Mwaka huu ndo umekuwa Mwisho kwao kujihusisha na Sifa
Mbaya Mitaani ikiwema Mabifu ya hapa na Pale ambayo yanaweza kuwaletea Sifa
Mbaya kwa mashabiki.
Pia wameongeza kuwa, badala yake
watajikita zaidi kuchomoa Mikwaju Mikali ambayo itawapa Heshima katika Muziki
wao unaowika zaidi Kimataifa.
Ili kuthibitisha hilo, majembe hao
wa SWEETER THAN KUKU waliingia katika page yao ya Facebook na kuandika kuwa wasanii
wanatakiwa kutoa Muziki Mzuri na Mkali kwa ajili ya Jamii, na Sio kujihusisha
na matukio mabaya, kwani haijengi Muziki Mzuri. Hivyo kwa Mwaka huu wamemaliza
Tofauti zao na BEBE COOL pamoja na JOSEE CHAMELEONE, hivyo hawana beef hata
kidogo, so wako katika Mahusiano Mazuri.
EmoticonEmoticon