Pengine hii inaweza ikawa ni
ahueni katika Mishe chafu za kikorofi kwa Mdogo wetu huyu ambaye hivi sasa ni
talk of the world kwa Kufanya majanga Kibao. Sasa imekuwaje katika Kurambishwa
Mkataba Bila Yeye kupenda wala Kutarajia.. Zima.
Mkali wa Pop Nchini marekani
JUSTIN BIEBER alirambishwa Mkataba wa Kuwa na Nidhamu ya hali ya Juu Pindi
atakapokuwa katika Hotel moja iliyoko nchini New Zealand,
Kwa mujibu wa mitonyo wa wadakuzi
na wakuda waliokubuhu katika udaku, inasemekana kuwa, Bwana Bieber alipigwa
Bonge moja la Stop kuingiza wasichanakatika Chumba cha Hotel ya LANGHAM, alichokigharamikia kwa EURO 1000,
pamoja na kula Sehemu tofauti na Wageni wengine, ili kuepusha Tafrani ambazo
zinaweza Kujitokeza.
Kwa mujibu wa Chanzo cha Mtonyo
huu, inasemekana kuwa Mkataba huo Ungemuamuru Bwana Bieber Kusepa haraka bila
Ubishi endapo angekiuka masharti ya Mkataba.
Hata Hivyo, baada ya mkataba huo
wa nidhamu kwa majanga Boy Huyo Mwenye umri wa Miaka 19, Management yake
(Biebr) ililazimika kuusaini licha ya Kuwa na Msururu wa masharti ya kutosha,
kwani Utawala wa hoteli haujarishi Umaarufu wa Justin bieber, bali wao wanamchukulia
kama Mteja yeyote Yule anayekuja hapo
Pia mdaku huyo aliongeza kuwa,
Justin bieber hakuwa na Budi kukubaliana na maamuzi hayo, ambapo masharti
mengine makubwa mawili ni Kutokparty ndani ya hotel hiyo, ama kuwabugudhi wateja
wengine.
EmoticonEmoticon