Wengi huwa tunamfahamu Kanye West kama Mtu ambaye
huwa hapendi masihala na hata Kufuatwa fuatwa katika Mishe yake ya aina yeyote.
Lakini Siku kadhaa baada ya Kutoa Video yake
alomshirikisha Mchumba wake, Kim Karadshian, Jamaa wawili wanaofahamika kwa
majina ya JAMES FRANCO na SETH ROGEN walitoa Bound 3 wakirudia kile ambacho
Knaye na Kim Wamekifanya , ikiwa ni katika mfumo wa masihala Fulani
Lakini Baada ya Kanye West na Mchumba ake Huyo Kim
Kuiona Video hiyo, waliisifia na hata Kuipongeza kwa Kadri ambavyo Jamaa hao
wawili walitumia Ubunifu wao Wa Jinsia Moja, yaani Kanye Ni Mwanaume, na Kim ni
Mwanaume Pia.
Tofauti na Watu ambavyo walitarajia kuwa wawili hao
Kanye (36) na Kim (33) wanaweza kufungua mastaka na hata Kuwasakama James na
Seth, video hiyo ilipongezwa na hata Kupigiwa Promo ili iweze kutizamwa na Watu
ili wapate hata Fursa ya kucheka
Kupitia Account yake ya Twitter, Kim Kardashian
ambaye ni mama Wa Mtoto wa Kanye, North West, aliweza kutweet kwa kuwaambia
wameipatia na ilikuwa inafurahisha
Kim hakuishia hapo tu, bali alimtweet Seth Rogen na
kusema kwamba, kanye West amechekeshwa sana na Video hiyo.
Kwa Upande wake Seth Rogen alimshukuru Kim
kardashian kwa kuweza kuielewa kazi waliyoifanya
EmoticonEmoticon