Victoria Akionesha Kovu Lake kubwa katika Mguu
Victoria akionesha Sehemu nyingine
Victoria akionesha Makovu Mengine katika Mkono (PICHA ZOTE NA DJ. ALEX)
Na Frank Joachim & Dj Alex.
Licha Ya Kupigiwa kelele kila Siku, suala la Unyanyasaji bado linazidi kushika kasi katika Maeneo Mbali mbali.
VICTORIA LUMWA, alikutana na Mkasa ambao haukuwa na Maana ya kumpatia makovu yenye Mateso makali kama anayoyapata Hivi Sasa.
ANAISHI WAPI:
Victoria ni Mkazi wa jiji la Mwanza, na anaishi maeneo ya IGOMA. Binti huyu anaishi na Dada yake, ambaye ni Mlezi wake Kwa hivi sasa
KISA CHA KUKUTANA NA MKASA HUO:
Kwa Mujibu wa maellezo yake, kuna Kijana amekuwa akimtaka Kimapenzi kwa Muda Mrefu, jambo ambalo Binti huyu hakuwa tayari kulifanya kwa kuzingatia Hisia zake. Baada ya Victoria Kumkataa Kijana huyo, majibu yaliyotoka ni "Si Unajifanya unanikataa...sasa Ngoja utaona."
Kauli hiyo haikumshtua sana Binti huyu Mrembo wa Kiafrika, na kuamua kuendelea na Maisha yake ya kawaida. lakini siku moja wakati anasafisha Vyombo nyumbani kwa Dada yake, alishangaa Ghafla anatokea Mtu akiwa amebeba Sufuria, huku ndani yake kukiwa na maji ya Moto.
Baada ya Victoria kuhisi hali ya hatari, aliamua kujikinga na Mkono na Kugeukia ubavu mwingine, ili kuepusha maji hayo kumpata Usoni. Dhamira kubwa ya Mtendaji wa tukio hilo, ilikuwa mni Kumuunguza Victoria Usoni, ili kuiharibu Sura yake ambayo inasemekana kuwa ndiyo inayompatia Kiburi cha Kuwakataa wanaume.
IMANI ZA KISHIRIKINA :
Victoria anaamini kuna uwezekano wa Imani za Kishirikina kuhusika kwa namna moja ama nyingine. Sababu za Victoria kusema hayo ni :
- MTENDAJI wa Tukio hilo alikuja kimazingara, baada ya Kutokea Ukutani akiwa katika Mavazi ya ajabu na kuchukua hatua hiyo, kisha Kupotea Ghafla.
- Jamaa aliyemtongoza na kumtishia Hilo, ni Mkazi Wa KIGOMA, ambako KWA IMANI zake yeye (Victoria) anadai kuna Imani za Kishirikina
EmoticonEmoticon