Mtu aliyejifanya Kardinali wa Kanisa Katoliki, Ralph
Napierski (kushoto) akisalimiana na Kardinali Sergio Sebiastiana. Napierski
alikamatwa akijaribu kuingia kwenye mkutano wa makardinali unaoendelea Vatican
ASKOFU bandia amefanikiwa kujipenyeza na kuingia kwenye
mkutano wa makadinali unaoendelea mjini Vatican , kwa ajili ya maandalizi ya
uchaguzi wa Papa mpya.
Askofu huyo bandia, Ralph Napierski ambaye ni mzawa wa
Ujerumani alifanikiwa kujipenyeza na kusalimiana kisha kupiga picha za
kumbukumbu na baadhi ya makadinali waliopo kwenye mkutano huo bila kugundulika.
Uzamiaji wake ambao ulileta mashaka kuhusu uimara wa usalama
eneo hilo
wanapokutana makadinali 103, ambao wamekusajika kwenye Makao Makuu ya Kanisa
Katoliki kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Papa mpya, huku wengine 12
wakiwa hawajawasili.
Katika mkutano huo, Kadinali wa juu kutoka Uingereza, Cormac
Murphy O'Connor pia anahudhuria.
Napierski alionekana akisalimiana na Kadinali Sergio
Sebiastiana nje ya ukumbi wa Papa Paul VI akiwa hajatambua kuwa siyo miongoni
mwa wenzake, huku akiwa amezungukwa na makasisi wengine wa kanisa hilo ambao pia hawakuweza
kutambua.
Walinzi wa kundi la Swiss Guars linaloshughulika na ulinzi
wa Makao Makuu ya Kanisa Katoliki Vatican , walimbaini kuwa siyo miongoni mwa
wahusika kutokana na vazi lake
alilofunga kiunoni,
ambalo siyo sahihi bali ulikuwa ni mtandio uliokunjwa vizuri.
Pamoja na vazi hilo la rangi
ya zambarau kutokuwa sahihi, pia kofia aliyokuwa ameivaa haikuwa miongoni mwa
zile zinazotambulika kuvaliwa na viongozi wa kanisa hilo .
Tofauti nyingine iliyobainika ni ufupi wa kanzu yake na
rozari aliyovaa haikuwa halisi, kwa kuwa ilikuwa ni fupi kuliko wanazotumia
viongozi wa kanisa hilo .
Kabla ya kubainika, Napierski alijitambulisha kwa waandishi
wa habari kwamba jina lake
ni Basilius ni miongoni
mwa wawakilishi wa Kanisa la Orthodox kutoka Italia.
Awali, kulikuwa na taarifa kwamba aliwaeleza waandishi wa
habari kuwa Kanisa Katoliki limefanya “Kosa kubwa” kwa kuwaruhusu makasisi
wanaotuhumiwa kwa makosa ya ngono kubadilishwa kutoka maeneo yao ya awali na kupelekwa kwingine, kuficha
kashfa zao badala ya kuzishughulikia.
Mtuhumiw ahuyo ambaye baada ya kubainika aliondolewa eneo hilo , anaongoza tovuti ambayo aliitumia kujitambulisha
kwamba yeye ni kasisi kupitia Shirika la Kikatoliki la Corpus Dei, huku akiwa
amevaa mavazi ya kikasisi na kujidhihirisha kama “Mtumwa na Nabii kama Mtakatifu Paul”.
Msemaji wa Kanisa Katoliki mjini Vatican ,
Federico Lombardi alisema hayupo tayari kuzungumzia suala hilo kwa sababu hajapata taarifa yoyote na
muda wote alikuwa akishughulika katika
mkutano.
EmoticonEmoticon