KWA MUJIBU wa taarifa kwa taifa, makamu wa rais wa Venezuela
Nicholas Marduro ametangaza kufariki dunia kwa rais Hugo Chavez, 58, kufuatia
kuugua muda mrefu maradhi ya Saratani. Rais Chavez ametoweka katika hadhira ya
nchi hiyo kwa muda mrefu ambapo alikuwa anapokea matibabu nchi jirani ya Cuba .
Marehemu Chavezi alirejea , mjini Caracas mnamo Februari 18 kwa mara ya kwanza
tangu maradhi yake yamzidie ambapo alipelekwa hospitali ya kijeshi kuendelea
kupokea matibau. Hata hivyo maelezo zaidi hayakutolewa juu ya afya yake.
Waandamanaji waliandamana katika mji mkuu Caracas
mwishoni mwa juma wakidai kuwa watu wa
KUHUSU AFYA YAKE
Bwana Chavez amekuwa katika uongozi nchini Venezuela kwa
miaka 14 na anatazamiwa kuleta mageuzi makubwa yaliyolenga zaidi kuimarisha
maisha ya raia wa pato la chini.
UJUMBE KUTOKA KATIKA JESHI LA VENEZUELA
Taarifa kutoka kwa jeshi imesema kuwa wataendelea kuilinda
hadhi ya nchi na kuimarisha usalama. Pia jeshi limeahidi kuendelea kuwa
waaminifu kwa makamu wa rais Nicholas Marduro na wakatoa wito kwa raia kuwa
watulivu.
WASIFU WAKE
Hugo Chavez alijitosa katika siasa za Venezuela mnamo Februari 1992 akiwa
luteni katika jeshi. Aliongoza mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo Carlos
Andres Perez.
Lakini kutokana na kukosa usaidizi wa kutosha wa kijeshi,
Chavez na wanamgambo wenzake walishindwa kunyakua madaraka hayo. Alikiri
kushindwa na aliwekwa korokoroni.
Aliingia uongozini baada ya ushindi mkubwa ulioviondosha
vyama vya kisiasa wakati huo. Katika kuapishwa kwake mnamo February 1999, Hugo
Chavez alitangaza wazi kwamba mipango yake ya mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi
sio kampeni tu. Alitimiza ahadi yake na kuiongoza nchi hiyo katika mabadiliko
ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika muda wa miongo kadhaa. Alibadili muundo wa
bunge na kulifanya kuwa la kikatiba, ambalo liliiunda katiba mpya baada ya kura
ya maoni iliyoidhinishwa na 88% ya wapiga kura.
Rais Chavez alitaifisha rasilmali ukiwemo utajiri wake
mkubwa wa mafuta. Sera kama hizi zilimfanya
azozane na kampuni za kimataifa za mafuta, lakini alipata uungwaji mkono mkubwa
wa watu maskini.
MAHUSIANO YAKE NA NCHI NYINGINE KIMATAIFA
Kutokana na urafiki wake na viongozi wa mrengo wa kushoto
kama vile rais wa Cuba, Fidel Castro, ambaye walikuwa na uhusiano wa karibu
aligongana kidiplomasia na Marekani, ambayo ni mshirika wake mkuu wa
kibiashara.
Chavez alipendwa nyumbani na wafuasi wake lakini alipingwa
na baadhi ya watu nchini humo na katika nchi za nje. Alionekana sio tu kama
bingwa wa jamii maskini lakini pia kama
muingiliaji wa siasa za nchi jirani. Katika miaka ya hivi karibuni alilenga
kukabiliana na masuala ya ndani ya Venezuela ,
kama uhalifu, kuinua uchumi wa nchi na
kukabiliana na rushwa.
BBC
EmoticonEmoticon