TUNIS, Tunisia
Serikali ya mseto ya Tunisia inayooongozwa na harakati ya
Kiislamu ya an Nahdha imetangaza kuwa imekubali kuendesha chaguzi za rais na
bunge tarehe 23 mwezi Juni ambapo rais atachaguliwa moja kwa moja na wapiga
kura.
Makubaliano hayo yamejiri baada ya mrengo wa upinzani kukosoa vikali
kwamba harakati ya an Nahdha inataka kudhibiti serikali na kukwepa uchaguzi.
Harakati ya Kiislamu ya an Nahdha ya huko Tunisia ilishinda uchaguzi wa kwanza
huru nchini humo mwezi Oktoba mwaka jana kufuatia mapinduzi ya wananchi
yaliyomng'oa madarakani Rais Zainul Abidin bin Ali.
Serikali ya mseto ya
Tunisia imesema kuwa wamefikia makubaliano ya kuendesha chaguzi za rais na
bunge tarehe 23 mwezi Juni mwaka huu, na duru ya pili ya uchaguzi wa rais
tarehe saba Julai.
EmoticonEmoticon