A
Raisi wa Kenya, Mwai Kibaki, na Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton |
Na Frank M. Joachim & DW
Nairobi, KENYA
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani, Hillary Clinton,
ameitaka Kenya iendeshe uchaguzi huru na wa haki, ili iwe mfano wa kuigwa kwa
mataifa mengine duniani.
Clinton amezitaka mamlaka zinazohusika na kuandaa uchaguzi
wa mwakani, kuhakikisha kuwa nchi hiyo haitumbukii tena katika machafuko kama
yaliyotokea mwaka 2007, ambapo watu 1,200 waliauwa. Waziri Clinton alikutana na
rais Mwai Kibaki, ambaye kikatiba haruhusiwi kuogombea muhula mwingine, na
Waziri Mkuu Raila Odinga, anayeongoza katika kura za maoni kuelekea uchaguzi
huo.
Clinton alisema serikali ya Marekani iko tayari kuisiadia
Kenya kuhakikisha inaendesha uchaguzi huru na wa haki na kuwataka raia wote wa
Kenya kuungana pamoja na kuandaa uchaguzi utakaokuwa mfano wa kuigwa. Clinton,
aliyeko barani Afrika kwa zaira ya mataifa saba, alitarajiwa pia kukutana na
rais wa Somalia, Sheikh Sharif Ahmed, na maafisa wengine wa nchi hiyo, kabla ya
kuelekea Malawi na Afrika Kusini.
EmoticonEmoticon