Lagos, Nigeria
Na Frank M. Joachim.
Watu wenye silaha wameivamia mashua inayomilikiwa na kampuni
ya huduma za mafuta katika bandari ya Nigeria leo, na kuwateka nyara raia wanne
wa kigeni na kuwaua Wanigeria wawili.
Msemaji wa Jeshi la majini la Nigeria, Kabir Aliyu,
amethibitisha kutekwa kwa wataalamu hao wanne wa kigeni na kuuawa kwa mabaharia
wawili.
Pia ameongeza kuwa, uraia wa wageni waliyotekwa nyara bado
haujathibitishwa. Maafisa sita wa jeshi la majini, ambao wote ni raia wa
Nigeria walikuwepo kwenye mashua hiyo, ambayo inamilikiwa na kampuni ya Sea
truck Oil Services, kuhakikisha usalama.
Wawili kati yao waliuawa na wawili walijeruhiwa, alisema
Aliyu. Aliongeza kuwa jeshi la majini la Nigeria limetuma boti na helikopta
katika eneo la tukio.
EmoticonEmoticon