Kim Jong Un, Rais wa Korea Kaskazini |
Pyongyang, Mji Mkuu wa Korea Kaskazini. |
Na Frank M. Joachim & DW
Pyongyang, KOREA KASKAZINI
Korea ya Kaskazini inahitaji msaada wa haraka wa chakula,
baada ya mvua kubwa kuuwa idadi kubwa ya watu na kusababisha mafuriko katika
maeneo mengi ya kilimo.
Haya yametangazwa na afisa wa Umoja wa Mataifa jana, ambapo amesema ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji
mkuu wa Korea Kaskazini Pyongyang imethibitisha hali hiyo baada ya kuyazuru
maeneo yaliyoathirika mwanzoni mwa wiki.
Mvua kubwa iliyonyesha mara mbili iliuwa watu 119 na
kuharibu maelfu ya nyumba za watu, hii ikiwa ni kwa mujibu wa vyombo vya habari
vya serikali ya Korea Kaskazini. Marekani imesema inatathmini msaada inaoweza
kuutoa, ingawa haijapata ombi kutoka kwa Korea Kaskazini. Mvua hizo ambazo
zilifuatia kipindi kirefu cha ukame, imezusha wasiwasi juu ya uwezo wa Korea
Kaskazini kutosheleza mahitaji ya chakula kwa watu wake.
Mwezi Juni Umoja wa Mataifa ulisema theluthi mbili ya wakazi
milioni 24 wa Korea Kaskazini hawana chakula cha kutosha.
EmoticonEmoticon