Moja kati ya Meli Hatari za Kivita za URUSI. |
Na Frank M. Joachim & DW
Moscow, URUSI.
Watu wengi wameuawa katika mitaa ya mji wa Hama ulio
katikati mwa Syria, ambao umezingirwa na wanajeshi wa serikali.
Ripoti hii ni kwa mujibu wa Shirika la Kuchunguza Haki za
Binadamu la nchini Syria lenye makao yake nchini Uingereza. Shirika hilo
halikutaja idadi kamili ya waliokufa, likisema mawasiliano ya simu katika
wilaya ya Al-Arbaeen yalikuwa yamekatwa.
Hata hivyo, Kamati ya Kuratibu Shughuli za Wanaharakati imesema
waliokufa, ambao ni raia na waasi, hawapungui 50. Hakuna shirika lisiloegemea
upande wowote lililothibitisha idadi hiyo.
Msemaji wa Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Syria Hisham
Hassan amesema wameondoa wafanyakazi wao kwa kuhofia usalama. Huku hayo yakiarifiwa, Urusi imetuma meli
tatu kubwa za kivita nchini Syria, zenye kubeba nyambizi 120 kila moja.
Shirika la Habari la Urusi limemnukuu afisa wa Urusi
akithibitisha kutumwa kwa meli hizo, lakini sababu ya kile zinachokwenda
kukifanya haikutajwa. Wakati huo huo tangazo la kujiuzulu kwa mpatanishi wa
kimataifa nchini Syria Kofi Annan ifikapo mwishoni mwa mwezi huu, limechukuliwa
na wachambuzi kama kutoweka kwa uwezekano wa kupatikana kwa sulihisho la amani
katika mzozo wa Syria.
EmoticonEmoticon