Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki Nchini Tanzania, Mwadhama Polycap Kardinali Pengo |
TARIME, Musoma
PADRI wa Kanisa Katoliki Parokia ya Nyamwaga, wilayani hapa,
huenda akafikishwa mahakamani kwa madai ya kupora ardhi ya mwanakijiji mmoja,
John Zacharia.
Kwa mujibu wa notisi ya siku 30 iliyotolewa na wakili wa
mwanakijiji huyo, Mwehozi Charles kutoka kampuni ya sheria ya Nola, mteja wao
atalazimika kumshitaki padri huyo kwa kukiuka makubaliano ya awali kati ya
pande hizo.
Notisi hiyo inasomeka kuwa, pande hizo zilikubaliana
kuelewana nje ya mahakama katika kesi ya msingi Na 58/2011 katika baraza la
ardhi wilayani hapa, ambapo baada ya kufikia makubaliano ilikubaliwa kuwa padri
huyo angefidia ardhi na miche ya kahawa 350 iliyokuwamo.
Zacharia alidai kuwa baada ya kufikiwa makubaliano hayo,
hakutekeleza na badala yake akavamia eneo hilo na kuharibu miche hiyo na
kuhamishia mawe na mchanga eneo hilo bila fidia yoyote, hali iliyosababisha
hasara kubwa tofauti na makubaliano ya awali.
Inasemekana kuwa juhudi za kumchukulia hatua za kisheria
paroko huyo katika kituo cha polisi Nyamwaga hazijafua dafu kutokana na kukaidi
wito kutoka kwa mkuu wa kituo.
Alipotafutwa na gazeti hili, paroko huyo alidai hawezi
kuzungumza chochote kwa kuwa yeye si msemaji wa kanisa hilo, bali atafutwe
askofu wa Jimbo la Musoma.
EmoticonEmoticon