IGP Said Mwema
SHINYANGA
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Salumu Msangi alisema kuwa
mwanamke huyo, Hollo Mabula (28), alikamatwa Novemba 5 usiku saa tatu nyumbani
kwake katika Kijijji cha Ng’wang’wali, Kata ya Mwaswale.
Alisema kuwa mwanamke huyo anayesadikiwa kuwa mmoja wa
majambazi, alikamatwa na bunduki hiyo aina ya G.3 ikiwa na risasi zake 35 na
risasi zingine 99 za SMG ambazo pia zinaweza kutumika katika bundukia aina ya
SAR, alizokuwa amezihifadhi nyumbani kwake.
Kamanda alifafanua kuwa bunduki hiyo ilikuwa imefichwa chini
ya uvungu wa kitanda chake ikiwa na idadi hiyo ya risasi na zingine zikiwa
zimewekwa ndani ya soksi na kutundikwa juu ya dari.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa akiitumia silaha hiyo
iliyofutwa namba zake katika vitendo vya ujambazi na ujangili ndani ya hifadhi
ya Serengeti, Maswa Game Reserve na maeneo mengine.
Kamanda alifafanua kuwa, hata mume wa mwanamke huyo, Masanja
Maguzu, aliwahi kukamatwa na bunduki ya SMG na risasi 622 na kufungwa jela
miaka 15.
EmoticonEmoticon