KAMPALA, UGANDA
Serikali ya Uganda imelitaka kundi la M23 la Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo lisianzishe tena mapigano ambayo yamewalazimisha maelfu
ya wakimbizi wa Kikongo kuvuka mpaka na kuingia nchini Uganda.
Wito huo
umetolewa na Okello Oryem, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uganda ikiwa ni siku
moja tu baada ya Harakati ya Waasi ya M23 kutishia kwamba, itaanzisha tena
mashambulio dhidi ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Okello Oryem amesema, Kampala inalitaka kundi hilo kuheshimu usitishaji mapigano.
Kundi la M23 lilisitisha mapigano Agosti mwaka huu baada ya kukutana na Rais
Yoweri Museveni mjini Kampala na kutakiwa kufanya mazungumzo na serikali ya
Kinshasa.
Hata hivyo Runninga Lugerero, mmoja wa viongozi waandamizi wa M23
alitishia mwishoni mwa juma akiwa huko Bunagana kwamba, kundi lao litaanzisha
tena vita kutokana na kuwa, Rais Joseph Kabila wa Kongo hayuko tayari kufanya
mazungumzo ya amani.
EmoticonEmoticon