Sudan Kaskazini na Sudan Kusini zimefikia makubaliano ya usalama wa
mpaka na usafirishaji mafuta baada ya mazungumzo ya siku nne katika mji mkuu wa
Ethiopia, Addis Ababa.
Rais Omar al Bashir wa Sudan na mwenzake Salva Kiir wa Sudan
Kusini ambao wamekutana mara 6 tangu Jumapili iliyopita wanatarajiwa kutia
saini makubaliano hayo leo Alhamisi. Makubaliano hayo yatafungua njia ya kuanza
tena usafirishaji mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba ya Sudan.
Hata hivyo
nchi hizo mbili zimeshindwa kuafikiana juu ya masaula kadhaa yanayohusu mpaka.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Sudan El Obeid Morawah amesema masuala
hayo yatajadiliwa katika siku zijazo.
Nchi hizo mbili zimekuwa zikishinikizwa na Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa kumaliza hitilafu zao.
EmoticonEmoticon