ASKARI WA JESHI LA KENYA AKIWA KAZINI |
Kenya imesema kuwa jeshi lake la majini limeshambulia vituo vya waasi wa
kundi la as Shabab katika bandari ya Kismayu huko kusini mwa Somalia, kabla ya
kufanywa mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya waasi hao.
Msemaji wa jeshi la Kenya Cyrus Oguna amesema, kikosi cha majini cha Kenya
kimefanya mashambulizi hayo baada ya vikosi vya anga kulenga ghala la silaha
karibu na uwanja wa ndege wa Kismayu.
NEMBO YA KUNDI LA AL- SHABAAB |
Oguna ameongeza kwamba, shambulizi hizo
linaonyesha jinsi jeshi la Kenya lilivyoshadidisha operesheni zake huko Kismayu
na kwamba mashambulizi ya nchi kavu bado hayajaanza.
Msemaji huo wa jeshi la
Kenya amesema, askari wa nchi hiyo wanatarajiwa kuanza kuingia Kismayo wakati
wowote mwafaka kuanzia sasa.
KUNDI LA AL- SHABAAB |
Vikosi vya jeshi la Kenya vikishirikiana na askari wa Burundi, Uganda na
Djibouti kwa wiki kadhaa vimekuwa vikipambana na waasi wa as Shabab katika
operesheni inayofanyika chini ya mwamvuli wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja
wa Afrika nchini Somalia AMISOM.
Askari hao wamefanikiwa kuwafurusha waasi hao
kutoka katika ngome zao.
EmoticonEmoticon