Na Frank M. Joachim.
Habari kutoka eneo la Tana River nchini Kenya zinasema kuwa
idadi ya watu waliouawa kwenye machafuko ya kikabila katika eneo hilo imepanda
na kufikia 40.
Maafisa 9 wa polisi
ni miongoni mwa waliouawa kwenye ghasia hizo. Kitovu cha machafuko hayo ni
katika kijiji cha Kilelengwani ambapo magari kadhaa ya polisi yamechomwa moto
na vituo kadhaa kuharibiwa. Makabila ya Pokomo na Ormo yamekuwa yakipigania
ardhi ya malisho kwa muda mrefu na mwishoni mwa mwezi uliopita mvutano huo wa
ardhi uligeuka na kuwa mapigano ya silaha.
Utulivu wa kiasi
fulani ulirejea lakini mwanzoni mwa wiki iliyopita, machafuko hayo yakaanza
upya. Habari zaidi zinasema mamia ya watu wamejeruhiwa kwenye ghasia hizo.
Maafisa zaidi wa usalama wamepelekwa katika eneo hilo ili
kutuliza hali ya mambo lakini wakazi wameilaumu serikali kwa kushindwa
kuwalinda pamoja na mali zao.
EmoticonEmoticon