Na Frank M Joachim
Bunge la Somalia leo linapiga kura ya kumchagua rais katika
uchaguzi ambao umetajwa na Umoja wa Mataifa kuwa ni wa kihistoria.
Uchaguzi huo wa rais
ambao umeakhirishwa mara kadhaa umetajwa kuwa na umuhimu mkubwa na ambao
utafungua ukurasa mpya wa kisiasa katika nchi hiyo ya Pembe ya afrika.
Balozi Augustine Mahiga mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa
amesema kuwa, uchaguzi huo ni wa kihistoria na una umuhimu mkubwa katika
kusukuma mbele juhudi za kuunda serikali mpya katika nchi hiyo iliyoharibiwa
vibaya na vita.
Wawakilishi wa Bunge
jipya la Somalia ambao wamechaguliwa siku chache zilizopita kutoka makundi
kadhaa ya nchi hiyo wakiwemo viongozi wa makabila, ndio watakaopiga kura za
kumchagua rais. Licha ya wanasiasa kadhaa wa Somalia kujitokeza kugombea kiti
hicho cha rais, lakini ushindani mkubwa unatarajiwa kuwa kati ya rais wa sasa
Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, Spika anayemaliza muda wake Sharif Hassan Sheikh
Aden na Waziri Mkuu Abdiweli Mohammad Ali.
EmoticonEmoticon