WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
JAY Z AJIBU SWALI KUHUSU UJAUZITO WA BEYONCE
Lile Vuguvugu lilovumishwa Hivi Majuzi kuwa Mwanadada Beyonce ni Mjamzito linazidi kuchukua Sura Mpya.
Baada ya Mama Mkwe wake Jay Z, yaani mama Mzazi wa Beyonce kukana Kuwa Binti yake huyo hana Ujauzito, Mume wake na Msanii Mkali wa HIP HOP pande za U.S of A, JAY Z "JIGGA" mekanusha vikali kuwa "NO PREGNANCY" kwa Mke wake Beyonce
Kwa Mujibu wa Muzungumzo na Chombo Kimoja nchini humo, Jayz alikataa kata kata kuwa Beyonce hana Ujauzito.
Mazungumzo yao yalikuwa Kama hivi :
MDAKU : "Vipi? Unamtoto Mwingine?
JAY Z : "Unamaanisha Usiku Huu?...Hapana !!"
MDAKU : "Vipi Kuhusu Miezi 9 Ijayo?"
JAY Z : "Hapana..Sio Miezi 9 Ijayo "
MDAKU : Kabla ya Miezi 9 Je?...yaani Miezi 7 au 8 Ijayo?"
JAY Z : Hapana !. Sio kabla au baada ya Mwezi Mmoja, Miwili, Mitatu, Minne,
Mitano, Sita, Saba, Nane au Tisa
"SIKUFANYA MAPENZI NA DIRECTOR WANGU"- CHRISTEN STEWART
Ikiwa ni katika Jitihada za Kumfanya Mpenzi wake Robert Pattinson kumuamin kama Mwanzo, Muigizaji Mdogo aliyekumbana na Skendo la "KU-NINONINO" na Director Wake Rupert Sanders...amekiri kuwa hakufanya Mapenzi na Director Huyo.
Muigizaji wa Filam ya THE SNOW WHITE, Christen Stewart, amemwambia Mpenzi wake kwa kumthibitishia kuwa Hata Siku moja hakuwahi "Kumfunulia Sketi" Director Huyo licha ya kukumbwa na Kashfa Hiyo
"Rupert hajawahi Kuchungulia Undani wangu licha ya kukumbwa na Skendo kali hiyo" Alilalama Mwanadada Christen Stewart.
Aidha imebainika kuwa, licha ya Usaliti uliofanywa na Mwanadada huyo, hivi sasa wamerudiana (Robert Pattinson na Christen Stewart- Katika Picha Hiyo Juu) tena, na Hivi sasa wanaishi Pamoja kama Mwanzo.
CONFIRMED : MAANDALIZI YA VIDEO YA "WANANUNA" YA SALVI MANYIKA NI MOTO WA KUOTEA MBALI....
SIMON MANYIKA "Salvy Boy"
Kichwa Matata kunako Muziki Wa Kizazi Kipya "Bongo Flava" hapa hapa U.R. of T (United Republic of Tanzania) SIMON MANYIKA goez by the a.k.a "SALVY MANYIKA" anatarajia kushusha Mzigo mwingine utakaokwenda kwa Jina la WANANUNA.
Hivi karibuni Mkali huyo wa Track ya "YASIKISA" ambayo inang'ara vilivyo kunako Media Kibao hapa Area 255, amepost baadhi ya SCENE zilizokuwa zikifanyika katika Video yake Hiyo Mpya katika Fan Page yake ya FACEBOOK.
MIKWAJU MINGINE YA SALVI MANYIKA.
1. UKO MBALI NAMI- Ft. Nemo
2. TUTASHUKURU.
3. YASIKISA
RICK ROSS IN DA BUILDING !!!!!.HAPA HAPA BONGO
MGUU PAAAAAAH......MPAKA CLOUDS TV, Si ndio nikakutana na BO...,BO...BO...BO...BONGE LA PROMOOOO!!!!
Eti kwamba....Wale wakali wa Matamasha U.R. of T. (United Republic Of Tanzania) namaanisha Area 255-Bongo...Clouds Entertainments Group, kupitia SERENGETI FIESTA 2012...BHAAAAAAAAAAAAAAAASSS...watamdondosha "Teflon Don, The Big Bous, Rozay" akifahamainka kama RICK ROSS hapa Bongo.
SUDAN KUSINI NA SUDANI KASKAZINI ZAFIKIA MAKUBALIANO
Sudan Kaskazini na Sudan Kusini zimefikia makubaliano ya usalama wa
mpaka na usafirishaji mafuta baada ya mazungumzo ya siku nne katika mji mkuu wa
Ethiopia, Addis Ababa.
Rais Omar al Bashir wa Sudan na mwenzake Salva Kiir wa Sudan
Kusini ambao wamekutana mara 6 tangu Jumapili iliyopita wanatarajiwa kutia
saini makubaliano hayo leo Alhamisi. Makubaliano hayo yatafungua njia ya kuanza
tena usafirishaji mafuta ya Sudan Kusini kupitia mabomba ya Sudan.
Hata hivyo
nchi hizo mbili zimeshindwa kuafikiana juu ya masaula kadhaa yanayohusu mpaka.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Sudan El Obeid Morawah amesema masuala
hayo yatajadiliwa katika siku zijazo.
Nchi hizo mbili zimekuwa zikishinikizwa na Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa kumaliza hitilafu zao.
KENYA WAIPIGA AL-SHABAAB TENA
ASKARI WA JESHI LA KENYA AKIWA KAZINI |
Kenya imesema kuwa jeshi lake la majini limeshambulia vituo vya waasi wa
kundi la as Shabab katika bandari ya Kismayu huko kusini mwa Somalia, kabla ya
kufanywa mashambulizi ya nchi kavu dhidi ya waasi hao.
Msemaji wa jeshi la Kenya Cyrus Oguna amesema, kikosi cha majini cha Kenya
kimefanya mashambulizi hayo baada ya vikosi vya anga kulenga ghala la silaha
karibu na uwanja wa ndege wa Kismayu.
NEMBO YA KUNDI LA AL- SHABAAB |
Oguna ameongeza kwamba, shambulizi hizo
linaonyesha jinsi jeshi la Kenya lilivyoshadidisha operesheni zake huko Kismayu
na kwamba mashambulizi ya nchi kavu bado hayajaanza.
Msemaji huo wa jeshi la
Kenya amesema, askari wa nchi hiyo wanatarajiwa kuanza kuingia Kismayo wakati
wowote mwafaka kuanzia sasa.
KUNDI LA AL- SHABAAB |
Vikosi vya jeshi la Kenya vikishirikiana na askari wa Burundi, Uganda na
Djibouti kwa wiki kadhaa vimekuwa vikipambana na waasi wa as Shabab katika
operesheni inayofanyika chini ya mwamvuli wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja
wa Afrika nchini Somalia AMISOM.
Askari hao wamefanikiwa kuwafurusha waasi hao
kutoka katika ngome zao.
Subscribe to:
Posts (Atom)