Na Frank M. Joachim & DW
Mripuko mkubwa wa gesi umetokea katika kiwanda cha kusafisha
mafuta nchini Venezuela na kuua watu 7 huku wengine 48 wakijeruhiwa. Mripuko
huo katika kiwanda cha Amuay kilichopo magharibi mwa nchi hiyo , umetokea
majira ya asubuhi, lakini gavana wa eneo hilo, ambaye amethibitisha vifo hivyo,
ameiambia televisheni ya taifa kuwa hali imedhibitiwa na kwamba hakutakuwa na
mripuko mwingine.
Kiwanda cha Amuay ni sehemu ya kituo cha usafishaji cha
Paraguana, ambacho ni moja ya vituo vikubwa zaidi vya usafishaji mafuta
duniani. Kiwanda hicho kina uwezo wa kusafisha mapipa 955,000 kwa siku. Waziri
wa nishati wa Venezuela, Rafael Ramirez amesema mripuko huo ulitokana na kuvuja
kwa gesi. Pia miundombinu ya kiwanda hicho imeharibiwa vibaya.
EmoticonEmoticon