I PAD YA APPLE
I PAD YA SAMSUNG
Na Frank M Joachim & DW
Mahakama ya mjini San Jose, katika jimbo la Kalifonia nchini
Marekani, imeiamrisha kampuni ya simu ya Samsung kuilipa kampuni ya Apple zaidi
ya dola bilioni moja, baada ya kugundulika kuwa kampuni hiyo ya Korea kaskazini
ilinakili sehemu muhimu za bidhaa za iPhone na iPad za Apple na kuzitumia
katika bidhaa zake za Galaxy.
Baraza la wazee katika mahakama hiyo lilitoa hukumu hiyo baada ya majadiliano ya siku mbili. Hii ni moja tu kati ya migogoro mingi ya kisheria kati ya makampuni hayo mawili ya kutengeneza vifaa vya elektroniki, na ambazo zinauza zaidi ya nusu ya simu za smartphone duniani kote.
Hukumu hii inaweza kusababisha kupigwa marufuku uuzaji wa bidhaa muhimu za Samsung nchini Marekani. Kufuatia uamuzi huo, mauzo ya hisa za Apple yalipanda kwa zaidi ya asilimia mbili katika muda wa saa mbili.

EmoticonEmoticon