Na Edwin Moshi.
Makete, NJOMBE.
Zikiwa Zimesalia siku Saba tu ,Imebainika kuwa maandalizi ya sensa ya watu na makazi
wilayani Makete yanaendelea vizuri hasa wakati huu ambapo mafunzo kwa
watekelezaji wa zoezi hilo yakiendelea kutolewa ngazi ya wilaya katika vituo
vinne tofauti
Hayo yamebainika leo wakati kamati ya sensa mkoa wa Njombe
ilipofanya ziara wilayani makete yenye lengo la kuangalia namna mafunzo kwenye
vituo hivyo yanavyoendelea ikiwa ni pamoja na kuelewa changamoto zinazowakabili
Mmoja wa wakufunzi katika kituo cha Bulongwa kinachojumuisha
tarafa mbili za Bulongwa na Magoma Bw. Fadhili Nkenza ameiambia kamati hiyo ya
mkoa kuwa mafunzo yanaenelea kutolewa na kwa wale wanapoatiwa mafunzo ya dodoso
refu kwa hivi sasa wanaendelea na mafunzo ya vitend ikiwemo kwenye kaya husika
Amesema katika kituo cha Bulongwa wanaopatiwa mafunzo kwa
dodoso refu ni 58 na wanapatiwa mafunzo ya dodoso fupi ni 53 na wote ni kutoka
kwenye tarafa mbili za Bulongwa na Magoma
Amesema kuwa kwa sasa wanandelea na mafunzo na wamefikia
kwenye hatua nzuri na ni lazima wayamalize kwa wakati kama ilivyopangwa kwenye
muongozo
Akizungumzia changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji
wa mafunzo hayo, Bw. Fadhili amezitaja kuwa ni pamoja na upungufu wa vifaa
(vifutio na penseli aina ya 2HB), mabegi kwa ajili ya kutunzia vifaa
walivyokabidhiwa makarani hao wa sensa, pamoja na majina ya watu maarufu
yaliyoandikwa kwenye ramani kukosewa hivyo kuwa ngumu kuwatambua ama kuwapata
watu hao
“kuna ramani tulizopewa zenye kuonesha maeneo mbalimbali
lakini katika ramani hiyo kumeandikwa majina ya watu maarufu hivyo majina
mengine yamekosewa kwa mafano unakuta mtu huyo maarufu amaitwa Fadhili Sanga
lakini kwenye ramani pameandikwa Fadhili Chaula, sasa huo ni mkanganyiko pindi
unapomtafuta humpati” alisema Fadhili
Ameongeza changamoto nyingine kuwa ni pamoja na malipo ya
darasa la dodoso refu kuchelewa, hamasa kwa jamii kuwa ndogo, baadhi ya
viongozi kutofahamu maeneo mengi wanayoyaongoza, ukubwa wa kazi lakini malipo
ni kidogo, E.A kuvuka mipaka ya kata (kwa kata ya Kipagalo na Bulongwa) pamoja
na changamoto ya wengi kusafiri kwa usafiri wa pikipiki na magari binafsi, hali
inayopelekea usumbufu wakati wa kurejshewa nauli zao kwani hawana risiti
kutokana na maeneo wanayotoka kukosa usafiri wa basi
Pia ameitaka kamati hiyo ya sensa wilaya kuangalia namna ya
kuwasaidia wakufunzi hao kutolipwa sawa na wanaopatiwa mafunzo kutokana na kazi
wanayoifanya wakufunzi hao ni kubwa lakini wanalipwa sawa
“Sisi wakufunzi tunatoa mitihani, bado tunabaki usiku
tukiisahihisha na pia muda wote tunatoa mafunzo tukiwa tumesimama, kwa kweli
tuoneeni huruma, lipelekeni hili mkoani muone namna ya kufanya kwa kweli”
alisema Fadhili
Hata hivyo kamati hiyo imesema itazifikisha mara moja
changamoto hizo mkoani na kuona namna ya kuzitatua kwani lengo ni kufanikisha
zoezi la sensa kama ilivyopangwa na serikali, huku ikiwataka wakufunzi hao
kutekeleza majukumu yao kwa kadri ya uwezo wao kwa sasa licha ya changamoto zinazowakabili
Kamati hiyo kwa hii leo imetembelea vituo viwili vya Iwawa
na Bulongwa
EmoticonEmoticon