Syria imekiri kwa mara ya kwanza kuwa inamiliki silaha za
kemikali na kibaolojia ambazo ingezitumia kama mataifa ya
nje yangeivamia kijeshi.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Kigeni ya nchi hiyo Jihaddi al-Makdissi amewaambia
waandishi wa habari kwenye mkutano kuwa kamwe silaha
hizo haziwezi kutumika dhidi ya waasi lakini zinaweza
kuzitumiwa kujibu mashambulizi kutoka nje.
Bashar Al Asad, Rais Wa Syria |
Waziri wa
Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema
kuwa kitendo hicho cha kutishia kutumia silaha kama hizo
ni cha kushitua. Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Ban Ki Moon amesema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuwa
huenda Syria ikashawishika kuzitumia silaha hizo.
Nchi hiyo
haijasaini mkataba wa kimataifa wa mwaka 1992
unaokataza kutengeneza, kutumia au kuwa na shehena ya
silaha za kemikali.
Hapo siku za nyuma, maafisa wa nchi
hiyo walikana kuwa na silaha za aina hiyo.
EmoticonEmoticon