Mafuriko makubwa yamelikumba eneo la katikati ya Nigeria na kuuwa watu 35. Mvua kubwa ilinyesha kwenye jimbo la Plateau usiku mzima wa jana na kuharibu nyumba 200.
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan |
Shirika la msalaba mwekundu kwenye eneo hilo linaripoti
kuwa miili hiyo imeshapatikana akiwemo mzee wa miaka 90
pamoja na mtoto wa miezi mitatu. Mkuu wa shirika hilo
Manasie Phampe amesema kuwa huenda idadi hiyo
ikaongezeka. Mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa pamoja
na maji kutoka kwenye bwawa lililofurika yalivisomba vijiji
kadhaa kwenye eneo la Jos ambalo ni makao makuu ya
jimbo la Plateau. Miili mengine 25 bado inatafutwa huku
mingi kati ya hiyo ikiwa ni ya watoto wenye umri wa miezi
mitatu hadi miaka 13 ambao walisombwa wakiwa usingizini.
Nigeria kwa sasa iko kwenye msimu wa mvua za mwaka
ambazo zimekuwa zikija na madhoruba yanayotoa
changamoto kwa maisha ya watu na miundombinu.
Mmoja wa Waathirika wa Mafuriko katika Nchi ya Nigeria |
Wiki
iliyopita watu watatu walikufa kutokana na mafuriko
kaskazini mwa Lagos kwenye eneo la Ibadan. Mwaka jana
pia watu 120 walikufa kwa mafuriko kwenye eneo hilo.
EmoticonEmoticon