REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANAMKE ALIYEPIGWA NA MSANII TREY SONGS AKIRI KUWA, WATU WALIKUWA WAMESIMAMA WAKATI ANAPEWA KIFINYO NA HAWAKUTOA MSAADA WOWOTE

2:08:00 AM

Na Rich Sam  
HATIMAYE Mwanamke ambaye alifungua Mashtaka dhidi ya Msanii Trey Songs kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi hadharani kisa  kaongea na mwanaume mwingine , ameamua kuweka wazi na kuanika namna ambavyo amejeruhiwa na Msanii huyo

Awali tulitoa Taarifa kuwa Trey Songs alifunguliwa mashtaka na Bibie ANDREA BUERA kwa kosa la kumpiga na kumjeruhi katika upande wa Parking walipokuwa wakitoka kula bata, huku tatizo kubwa likiwa ni bibie huyo kuongea na mwanaume, yaani kwa tafsiri ya Fasta ni kwamba, kulikuwa na Ishu ya WIVU

Akiwa na mwanasheria wake, Andrea aliweka wazi maeneo ambayo amejeruhiwa FEBRUARY 18 wakati wanatoka kunako After Party ya NBA ALL STARS WEEKEND na kudai kuwa ameamua kujitokeza mbele ya umma kuweka wazi kilichotokea ili uwe mfano bora hata kwa binti yake ambaye ana umri wa miaka 7

Katika Maelezo yake huku akitokwa na machozi, Andrea ambaye alikuwa ameambatana na Mwanasheria wake LISA BLOOM alizungumza haya, tunamnukuu

" Nilikuwa nimehudhuria After Party hiyo na ndipo Trey alianza kunifokea, kunikaba na kunipiga mitama na kunipiga ngumi na hata kunipiga mpaka nikaanguka Chini."

Kitu kilichoonesha kumuuma zaidi, ni namna ambavyo watu walishindwa kutoa msaada kwake wakati zoezi zima la kipigo kutoka kwa HIT MAKER huyo wa BOTTOMS UP linaendelea, tunamnukuu tena

"Watu walikuwa wamesimama tu na wanatazama namna ambavyo ninapewa kipigo. Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilichukua simu nimpigie mtu wa usafiri aje kunichukua, lakini alichukua simu yangu na kuipiga chini, halafu akachukua na simu yangu nyingine akafanya hivyo hivyo. Nililia sana katika Mshtuko mkubwa na nilitaka kwenda nyumbani

Nilijitahidi sana kwenda hosiptali kwa sababu aliniumiza sana, na hata nilipoamka usiku wa manane, bado nilikuwa nasumbuliwa na kumbu kumbu za ajabu na tukio lile"



Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER