Na Rich Sam
Wanaopenda Muziki wa HIP HOP watakuwa wanamfahamu vyema Kabisa Remy ma, moja kati ya Female Rappers wanaofanya vizuri sana na hata kusifika kupitia utamu wa Flow zake ambazo huwa anazitumia pindi anapoachia zigo
Lakini kuna Taarifa mbaya hasa kwa Remy Ma mwenyewe ikiwa ni baada ya Mdogo wake wa kike mwenye miaka 27, REMEESHA kukamatwa kwa kosa la kupiga Risasi katika Gari ambalo lilikuwa limebeba wanawake Watatu ndani yake
Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Jeshi la Polisi Nchini Marekani inadaiwa kuwa Tukio hilo lilifanyika Ijumaa ya juma lililopita, ambapo Rameesha ambaye ni mdogo wake na Rapper Remy Ma alifyatua Risasi katika Gari hilo huku wengi wakiwa hawajui sababu, hali iliyosababisha mtu mmoja kujeruhiwa.
Mmoja wa maafisa wa polisi anataarifu kuwa, baada ya Wanawake hao watatu waliokuwa katika gari iliyofyatuliwa Risasi kadhaa, walipanic na kuondoa gari , hali iliyosababisha mwanamke mmoja kugongwa na kujeruhiwa na Risasi
Baada ya Polisi kupata Taarifa hizo, walimkamata binti huyo anayefanana kabisa na Remy Ma siku ya Jumatatu ya Wiki hii nyumbani kwao.
Familia ilijitahidi kuweka dhamana kwa Rameesha, lakini ilishindikana kutokana na mambo mawili makubwa, MOJA ikiwa ni kuhofia kuhatarisha maisha ya Wahusika endapo angeachiwa huru, na MBILI ni kwamba, Rameesha awali alikuwa na kesi ya Kumdhuru mtu na silaha kali, na kupiga risasi kadhaa ndani ya jiji ikiwemo kumtishia mtu kwa Bastola
EmoticonEmoticon