Na Baba Juti
#WaungwanaWenzangu kama tukiulizana Neno "Kiki" limechukua trend kubwa Mwaka Gani, nadhani wengi tunafahamu ni kuanzia mwaka 2016 hivi mwishoni mpaka safari hii, ambapo pia ni kama linapoteza "utamu" hivi
Lakini pia kumekuwa na wengi hasa wasanii ambao waligundua kuwa Neno "Kiki" linweza kuwaletea Faida na hasara katika maisha yao na kazi zao kiujumla. Kiuhalisia, wapo waliopata faida kadhaa kutokana na Kik, lakini kuna wale waliaoambulia za Uso kutokana na Kiki
Leo, Shilole anawataka mjue na kufahamu kabisa, ikibidi muelewe kiundani zaidi kuwa Uhalisia wa Maisha Yake, Ndiyo Kiki yake, maana kuna wengine wameshatafsiri kuwa maisha yake anayatengeneza kumbe yeye ndiye uhalisia wake
Kupitia Instagram account yake, Shilole ambaye hivi sasa anajihusisha na muziki pamoja na biashara ya msosi, amesema kuwa yeye ana zari lake la kik hapa mjini, maana Maisha yake halisia, ni ndiyo Kiki Yake
Tunamnukuu
"Watu wenye zari na kiki zetu mjin 😂😂😂😂 wala sihangaikagi masikin ya Mungu ukweli wa maisha yangu ndo kiki yangu #usinitumiewatunjoomwenyeweUkitakawatuwakujuekavuenguokariakooo😂🖕"
EmoticonEmoticon