Na Rich Sam
#WatuWaMungu Huenda pia huu ukawa ni mwaka mgumu kidogo kwa mkongwe mwenye heshima kubwa katika Muziki wa Taratibu yaani R&B, R Kelly kutokana na hiki kingine ambacho kimemkuta
Baada ya kuandamwa na kashfa ya kubaka, kulawiti na kuteka na kufanya mapenzi na mabinti wenye Umri mdogo, safari hii pia kuna taarifa kuwa Mjengo wa Hitmaker huyo wa Track ya STORM IS OVER unaweza kupigwa mnada muda wowote kuanzia sasa
Taarifa kamili ambazo pia ni za uhakika zinadai kuwa, Mjengo huo ambao ulikuwa ukitumika katika matukio hayo ya ki-ngono na udhalilishaji bado una deni la nyuma ambalo ni USD 23,000 sawa na Tsh 52,785,000 ambapo Kodi ya mwezi kwenye jumba hilo ni USD 11,542 sawa na Tsh 26,488,890
Kutokana na sababu za kiuchunguzi, ilimbidi R.Kelly atolewe katika Nyumba hiyo kwa muda ili kufanya taratibu zakiusalama kuthibitisha kinachotuhumiwa.
Hata hivyo, Mhusika wa Mjengo huo aliamua kutoa Notice ya kumtaka R. Kelly aondoke katika nyumba hiyo ambayo iko GEORGIA, Marekani huku kukiwa na deni hilo, na hivi sasa "Father House" anataka kufungua mashtaka ya kulipwa Mpunga wake
EmoticonEmoticon