Na RICH SAM
Watu Wa Mungu mambo sio mazuri kwa upande wa Mkali wa Muziki wa Pop Nchini Marekani ambaye asili yake ni SENEGAL, hapa tunamzungumzia AKON
Hit Maker huyu wa DONT MATTER anatakiwa kuilipa kampuni ya GTFM Dolari za kimarekani 164,786.99, pesa ambazo anadaiwa kushindwa kuzilipa ikiwa ni baada ya kupanga katika Jengo lao kwa ajili ya matumizi ya biashara yake
Kwa Mujibu wa Vielelezo kutoka katika Kampuni hiyo, ni kwamba, Akon alienda katika Jengo la EMPIRE STATE (Empire State Building) akiomba kupangishwa Floor ya 66 kwa ajili ya Biashara yake ya masuala ya Fashion kupitia mavazi yake ya ALIAUNE MILANO.
Katika makubaliano yao, Akon alikubali kulipa USD 25,000 kwa mwezi, na alikuwa akilipa vizuri kuanzia JULY 2012 mpaka JULY 2015 ambapo inasemekana aliacha kulipa ghafla.
Kampui husika ikaongeza kuwa, AKON hakuwahi kulipa tena mpaka alipoondoka January 2016 akiwa anadaiwa deni la Takribani miezi saba.
Hata Hivyo, mahakama imebaini kuwa Akon ana makosa katika hilo na anatakiwa kulipa mkwanja anaodaiwa
EmoticonEmoticon