REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TAARIFA KUTOKA MAMLAKA YA MAWASILIANO-TCRA

12:13:00 AM




Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema
kampuni za simu za mikononi zinaruhusiwa kusajili upya laini kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kielektroniki inayohusisha uchukuaji wa alama za
vidole.


Kaimu meneja mawasiliano kwa umma wa mamlaka hiyo, Semu Mwakyanjala
alisema walishafanya majaribio kuhusu mfumo huo na kuona unafaa.

Mwakyanjala alitoa ufafanuzi huo baada ya mwandishi wa Mwananchi kuuliza
kuhusu ujumbe unaotumwa kwa wateja kutoka kampuni za simu za mkononi
ukiwajulisha kuhusu usajili wa laini kwa kutumia alama za vidole.

“Ndugu mteja katika kuboresha usajili wa laini za simu alama za vidole
zitatumika kuanzia Februari 5, 2018. Kwa mawasiliano zaidi tembelea
maduka yetu,” ni ujumbe ambao umekuwa ukitumwa kwa wateja wa kampuni za
simu.

Mwakyanjala alisema mfumo huo unaotumia alama za vidole na picha ni
wenye uhakika ambao ni vigumu kughushi.

“Huu ni usajili wa kielektroniki ambao unaiwezesha kampuni na mamlaka
kupata taarifa mbalimbali za mteja kwa muda mfupi,” alisema.

Alisema TCRA imeziruhusu kampuni zote za simu za mkononi kutumia mfumo huo.

Akizungumzia mfumo huo, meneja uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson
Mmbando alisema kampuni hiyo itaanza kusajili kwa majaribio.

“Ni kweli tutaanza kusajili laini kwa kutumia alama za vidole kwa sababu
hiyo ndiyo njia salama ya usajili,” alisema.

Alisema katika mpango huo wa majaribio wataanza kusajili katika mikoa
minne ya Dar es Salaam, Pwani, Iringa na Singida. Pia, utafanyika
Zanzibar. “Katika mikoa hiyo tutaanza kusajili wateja wapya kwa kutumia
alama za vidole,” alisema.

Alisema baadaye wataendelea kwa wateja wengine hata ambao walishasajili
laini kupitia mfumo wa zamani. “Lengo ni kuboresha zaidi mfumo huu.” 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER