DMX |
Na Baba Juti
LICHA ya kukabiliwa na Mashtaka kadha wa kadha ya kiuhalifu na hata kupandishwa kizimbani mara kwa mara, hatimaye Hakimu amemruhusu Rapper DMX kusafiri na kufanya shughuli yake ya msingi
DMX ambaye hivi sasa ana Umri wa Miaka 47, anakabiliwa na Mashtaka ya kukwepa Kulipa Kodi huku Deni likiwa ni kubwa kiasi kwamba huenda ikamlazimu aishie Jela kutumikia Kifungo cha zaidi ya Miaka 6
DMX amekuwa akiandamwa na matukio mbali mbali ambayo inasadikika kuwa yameanza kumfanya asiwe sawa kisaikolojia |
Awali iliripotiwa kuwa, DM haturuhusiwa kutoka Nje ya Jiji la New York kutokana na Makosa ambayo yanamkabili, lakini hivi majuzi, hakimu ambaye anaendesha Kesi yake, amemruhusu Rapper Huyo Mkongwe kutoka New York na kwenda Hawaii kwa ajili ya Perfomance ya Show yake iliyoandaliwa huko
Ukiachilia mbali Perfomance hiyo ya Hawaii, DMX pia ameruhusiwa kuisafiri kwenda St Louis hapo Baadae mwezi huu, kwa ajili ya Perfomance yake pia, lakini kwa kuwa yuko chini ya Uangalizi, basi ataambata na Mshauri wake katika Gari lake kwa ajili ya uangalizi zaidi
EmoticonEmoticon